Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum akiwa ameshika mwenge baada ya kufika mtaa wa Kisutu jijini Dar kwe...
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akizungumza jambo mara baada ya
Mwenge wa Uhuru kufika eneo la Kisutu jijini Dar kwa ajili ya ufunguzi
wa Magari ya kisasa ya kuzoa taka.
Kiongozi
wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum akikata utepe
kuashiria ufunguzi rasmi wa magari ya kufanyia usafi yanayomilikiwa na
Kampuni ya Green Waste Pro ltd.
Meneja
mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw.Abdallah Mbena
akisoma risala kwa mgeni rasmi ambaye ni kiongonzi wa mbio za mwenge wa
uhuru kitaifa mwaka 2015 , Bw. Juma Khatibu Chum (hayupo pichani).
Kiongozi
wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum (kushoto)
akikabidhiwa risala na Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro
Ltd, Bw.Abdallah Mbena iliyosomwa wakati wa uzinduzi wa magari ya
kufanyia usafi katika manispaa ya Ilala jijini Dar.
Kiongozi
wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum (wa kwanza kushoto),
Mkurugenzi wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo
(katikati) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wakiwa
kwenye zoezi la kuweka uchafu kwenye moja ya gari la kufanyia usafi
lililozinduliwa na Mwenge wa Uhuru.
Mmoja
wa viongozi wa Mbio za Mwenge akizungumza mara baada ya uzinduzi wa
magari ya kufanyia usafi katika manispaa ya Ilala yanayomilikiwa na
Kampuni ya Green Waste Pro Ltd aliwasisitiza wananchi kuendelea kutumia
kampuni hiyo kwani usafi utaendelea kuimarika zaidi na zaidi.
Kiongozi
wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum(wa kwanza kushoto),
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (wa pili kutoka kushoto), Naibu
Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Kheri Kessy(katikati) Mkurugenzi wa Green
WastePro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo( wa pili kutoka kulia) pamoja na
Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw. Abdallah Mbena
wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa magari ya
kufanyia usafi katika eneo la Kisutu jijini Dar.
Mmoja
wa viongozi wa mbio za mwenge akiwa ameshikiria Mwenge wa Uhuru tayari
kwa kuondoka mara baada ya kumaliza uzinduzi wa magari ya kufanyia usafi
mali ya kampuni ya Green Waste Pro Ltd inayofanya kazi za usafi katika
manispaa ya Ilala jijini Dar.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ilala Ndugu Isaya M. Mngurumi (kushoto) akimsikiliza
Mkurugenzi wa Green Waste Pro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo akiwa na
Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw.Abdallah Mbena
wakiwa wanatoa maelezo juu ya uzoaji na usindikaji wa Taka
zinazokusanywa katika sehemu mbalimbali za Manispaa ya Ilala na jinsi ya
watakavyoyatumia magari hayo yaliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru.(Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog)
Akizungumza
wakati wakati wa tukio la uzinduzi wa magari ya kufanyia usafi ya
Kampuni iliyopewa zabuni kusafisha manispaa ya Ilala, Green Waste Pro
Ltd Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi amesema kushirikiana vyema
kwa kampuni Green Waste Pro Ltd ndiko kunako pelekea maendeleo na afya
bora katika manispaa ya Ilala hivyo tuwaunge mkono wenzetu kwa kuwapa
ushirikiano wa kuto tupa taka hovyo bali maeneo husika yaliyo wekwa
kwaajili ya kuhifadhi taka hizo ili waweze kuzipitia kwa urahisi na
kuzipeleka mahala panapo husika.
COMMENTS