MOAT YAUPINGA MSWADA WA SHERIA YA VYOMBO VYA HABARI DKT MENGI ANA KWA ANA NA ROSTAM AZIZI

Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi (kushoto), akisalimiana kwa kumbatiana n...








Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi (kushoto), akisalimiana kwa kumbatiana na Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Azizi ambaye pia ni mmoja wa wamiliki wa vyombo vya habari.



 Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Dk. Reginald Mengi (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mswada wa sheria ya vyombo vya habari ambao ulitaka kuwasilishwa bungeni kwa dharula. Kulia ni Mwanasheria, Godfrey Mpandikizi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Sahara Communication, Samuel Nyalla (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Saed Kubenea kutoka Mwanahalisi Publishers na Mwanasheria, Godfrey Mpandikizi.

 

 Wadau na wamiliki wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wanahabari na wadau wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo.
wadau wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo.


Na Dotto Mwaibale

WAMILIKI wa Vyombo vya habari nchini (MOAT) wameitaka serikali kutosaini muswada wa vyombo vya habari kutokana na kutokuwa wa haki na kwamba unavibana vyombo vya habari.

Pia wamiliki hao wamesema kama serikali inataka kuupitisha isubiri Rais ajaye ndiyo aupitishe wakati huohuo wameunda kamati maalumu itakayoenda Mjini Dodoma kuuzuia usipitishwe wala kujadiliwa bungeni.

Akizungumza Dar es Salaam leo mchana Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Regnald Mengi  alisema anashangazwa sana na wanasisa kusahau walipotoka kutokana na kusapoti muswada huo kupitishwa.

Alisema serikali imeamua kufanya hivyo kutokana na kusahau waliowasababishia kupata madaraka kutokana na shida yao kuisha hivyo vyomba vya habari vimejifunza.

"Tumejifunza kuwa sisi ni8 watu wa kutumika  wanapotaka kututumia hivyo wanataka kutumaliza na muswada huu hivyo sioni kama wana nia njema na sisi, "Alisema Mengi.

Aliongeza nia ya kupitishwa kwa muswada huo so njema na kwamba haki ya kupata habari sio tuu haki ya msingio bali ni ya kikatiba hivyo serikali isije ikajihusiasha na kuvunja katiba ya nchi bali inatakiwa kuonesha mfano bora.

Akizungumzia kuhusu Demokrasia alisema mtu hawezi kufanya vitu visivyozingatia demokrasia ili kudhibiti demokrasia au kuhakikisha unapata demokrasia kwa kutumia njia za kidemopkrasia bali anapaswa kutumia amani.

"Huwezio kuheshimu sheria kwa kutumia nguvu, hivyo muswada ukiwa na sheria onevu na isiyokubalika au kukiuka katiba ya nchi lazima hali itakuwa mbaya nchini,"

Kwa upande wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu alisema watanzania tunaelekea kwenye mchakato huo lakini hatuwezi kuwa na uchaguzi huru ikiwa vyombo vya habari havina uhuru wa kupokea na kuandika habari ili watanzania waweze kuelewa hivyo serikali inatakiwa kujadili kwa makini ili kunusuru machafuko yanayoweza kujitokeza.

"Hatuwezi kuficha vitu wakati mambo yanatakiwa yawe wazi, na kama tungekuwa tunataka uwazi tusingeruhusu vyombo vya habari kuwa wazi, hivyo muswada huo utatupa matatizo kwenye uchaguzi na hauwezi kluwa huru pasipo wananchi kujua nuini kinaendelea kupitia vyombo hivyo,"alisema Mengi. 

Hata hivyo mengi aliongeza kuwa hakuna amani endelevu bila kuwepo uhuru na haki kwa kuwa ni rasilimali kubwa ya taifa na kwamba si ya mtu mmoja, kikundi wala chama bali ni yetu sote hivyo serikali ikijaribu kuichezea itakuwa inacjhezea wananchi wa tanzania.

Kwa upande wake Wakili wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Godfrey Mpandikizi  akizungumzia changamoto zilizopo kwenye muswada huo,alisema vitu vilivyopo kwenye muswada huo vinakinzana na katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania hivyo aliwataka wahariri kwenda Dodoma kuuzuia.

Alisema muswada huo pia unazuia jamii kujua mambo yanayoendelea hivyo itasababisha hali ya nchi kuwa mbaya kwa siku zijazo kurtokana na kuwa na mapungufu zaidi ya 10 katika kila kifungu pamoja na tafsiri zaidi ya 20.

"Sheria hiyo ni chafu, na hairuhusiwi kwenda Bungeni hivyo isubiri Rais ajaye na katiba mpya ndiyo ujadiliwe ili uwe na haki hivyo wamiliki nendeni Dodoma mkauzuie usijadiliwe na wabunge kupitishwa,"alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mwananchi, Francis Nanai aliwataka wamiliki hao kuonana na wanasheria, wabunge na mashirika mengine kwenda mahakani kupinga sheria hiyo chafu.

Abdalah Majura alisema anaungana na vyombo mbalimbali vya habari kuukataa muswada huo usijadiliwe Bungeni na kwamba utasababisha kufa kwa taaluma za uandishi wa habari. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)




COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MOAT YAUPINGA MSWADA WA SHERIA YA VYOMBO VYA HABARI DKT MENGI ANA KWA ANA NA ROSTAM AZIZI
MOAT YAUPINGA MSWADA WA SHERIA YA VYOMBO VYA HABARI DKT MENGI ANA KWA ANA NA ROSTAM AZIZI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEinVwWcaA7I43MDn-dJhKZiKeywBtsOuT-AI6FpPXtI_szyZYt0CclJ8MQUfdUR8mHmOnG6C0N0SVcVyb8NpTZzATMQAQEj610KZC00fR_Xn59BUaACbnYRuSoD4KNZUyM7edVCP_HnX4w/s640/3.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEinVwWcaA7I43MDn-dJhKZiKeywBtsOuT-AI6FpPXtI_szyZYt0CclJ8MQUfdUR8mHmOnG6C0N0SVcVyb8NpTZzATMQAQEj610KZC00fR_Xn59BUaACbnYRuSoD4KNZUyM7edVCP_HnX4w/s72-c/3.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2015/05/moat-yaupinga-mswada-wa-sheria-ya.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/05/moat-yaupinga-mswada-wa-sheria-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy