BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, LIU DONG AZINDUA TAMTHILIA YA TUOANE 'LETS GET MARRIED

  Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Dong akitoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa Tamthilia mpya ya Tuonae, Lets Get Married il...








 Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Dong akitoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa Tamthilia mpya ya Tuonae, Lets Get Married iliyichezwa na wachina na kutafsiriwa kwa kiswahili. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar e Salaam jana. Kulia ni Ofisa kutoka ubalozi wa China, ambaye alikuwa ni mkalimani wa balozi huyo, Yetianfa Attache.
  Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Dong (kulia), akipeana mkono na Balozi wa StarTimes nchini, Msanii Nurdin Bilal 'Shetta' wakati wa uzinduzi wa Tamthilia hiyo.
Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Dong (kulia), akipeana mkono na Balozi wa StarTimes nchini, Msanii Nurdin Bilal 'Shetta' wakati wa uzinduzi wa Tamthilia hiyo.


 Maofisa wa Kampuni ya StarTimes wakifurahia jambo kwenye uzinduzi huo.
 Wanahabari wakichukua tukio hilo.
 Warembo wa StarTimes wakiwa tayari kwa zoezi la kuzindua Tamthilia hiyo. Kutoka (kulia) ni Hadija Saidi, Nyachilo Bunini na Fausta Mushi.
 Balozi wa StarTimes nchini, Msanii Nurdin Bilal 'Shetta'  (katikati), akiwa na wadau wengine kwenye uzinduzi huo.

Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.


Na Dotto Mwaibale


BALOZI wa China nchini Tanzania, Liu Dang amesema ushiriano wa kirafiki baina ya Tanzania na China ni muhimu sana katika ukuzaji wa sekta ya utamaduni.


Kauli hiyo aliitoa wakati akihutubia katika uzinduzi wa Tamthilia ya Tuonane 'Lets Get Married iliyochezwa na wachina baada ya kutafsiriwa kwa lugha ya kiswahili.


"China na Tanzania ndugu na ushirikiano na ubadishilianaji katika sekta mbalimbali hasa sekta  ya kiutamaduni zinahistoria ndefu hivyo zinapaswa kudumishwa" alisema Balozi Dong.


Alisema Rais wa China Xi Jingping alipotembelea Tanzania mwaka jana serikali za hizi nchi mbili zilipeana vizuri mawazo na kusaini mikataba mingi mbalimbali ya ushirikiano ambapo ziara hiyo iliziletea nchi hizi mbili mafanikio makubwa na kufungua ukurasa mpya wa maendeleo ya historia ya uhusiano baina yao.


Akizungumza katika uzinduzi huo Mchambuzi wa Vipindi wa Kampuni ya StarTimes Tanzania, Rehema Kisyombe alisema kutokana na ushiriano mzuri wa nchi hizo kwa upande wao StarTimes wameadhimia kuudumisha kwa njia ya burudani kwa kuleta vipindi mbalimbali kutoka china.


Alisema kwa kutambua hilo StarTimes imekuwa ikileta tamthilia mbalimbali za kichina zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ambapo mpaka hizi sasa wamekwisha onesha nne kupitia chaneli ya Kiswahili ijulikanayo kwa jina la Star Swahili.


Kisyombe alizitaja tamthilia hizo kuwa ni Mapambano, Ujana wangu, Matumaini ya Baba na Hot Mom ambazo zilipokelewa vizuri na watamazaji wa chaneli hiyo na sasa wanawaletea tamthilia hiyo ya Tuoane. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)



COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, LIU DONG AZINDUA TAMTHILIA YA TUOANE 'LETS GET MARRIED
BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, LIU DONG AZINDUA TAMTHILIA YA TUOANE 'LETS GET MARRIED
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiVBmtWn14jAQh5mYl7NfQzWDowLRlXgSDY9n__4UBM-0e3_lYTMHdkdxo5dTeogCyJ_fa5z-kkrAs_LkOg83QZwuX3dpEbr4qYYpTOtcrCNkFHjBioXC11A7jQfNkFq3iExX2kq-K5Oz8/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiVBmtWn14jAQh5mYl7NfQzWDowLRlXgSDY9n__4UBM-0e3_lYTMHdkdxo5dTeogCyJ_fa5z-kkrAs_LkOg83QZwuX3dpEbr4qYYpTOtcrCNkFHjBioXC11A7jQfNkFq3iExX2kq-K5Oz8/s72-c/1.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2015/05/balozi-wa-china-nchini-tanzania-liu.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/05/balozi-wa-china-nchini-tanzania-liu.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy