MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AONGOZA UPANDAJI MITI MABWEPANDE KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA KUPANDA MITI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki akipanda mti kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mji Mpya iliyopo Mabwepande nje kidog...








Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki akipanda mti kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mji Mpya iliyopo Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kwenye kilelele cha maadhimisho ya upandaji miti yaliyofanyika kimkoa wilayani Kinondoni leo. Wa tatu kulia anayeshuhudia upandaji miti huo ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.


 Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda akipanda mti katika maadhimisho hayo.
 Mratibu wa mazingira kutoka Taasisi ya EBPA, Charles Lugenga (kushoto), akitoa maelezo mbele ya mkuu wa mkoa na viongozi wengine wa Manispaa Kinondoni jinsi ya upandaji wa mimea mbalimbali pamoja na miti kwa kutumia matairi ya magari yaliyotumika.
 Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa wamebeba miche ya miti wakielekea kuipanda katika maeneo mbalimbali shuleni hapo.
 Wananchi mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo ya upandaji miti.
 Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa kwenye sherehe hiyo.
 Msanii akitoa burudani kwenye maadhimisho hayo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni akipanda mti.
 Diwani wa Kata ya Mabwepande, Clement Bocco  akipanda mti katika eneo la shule ya Mji Mpya.
 Mratibu wa mazingira kutoka Taasisi ya EBPA, Charles Lugenga (kushoto), akimpatia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki kikapu kilichotengenezwa kwa matairi yaliyotumika baada ya maadhimisho hayo.
 Wasanii wakitoa burudani.
 Maofisa wa Manispaa ya Kinondoni wakiwa kwenye 
maadhimisho hayo.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kushoto), na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda wakiserebuka pamoja na wananchi katika maadhimisho hayo ya upandaji miti mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika leo viwanja vya Shule ya Msingi Mji Mpya iliyopo Mabwepande.
Wananchi wakicheza segere baada ya kumalizika kwa zoezi 
hilo la upandaji miti.

Na Dotto Mwaibale

SERIKALI imesema waathirika wa mafuriko ya mto Msimbazi walioondoka baada ya kupewa viwanja maeneo ya Mabwepande na kurudi eneo la Msimbazi watanyang'anywa viwanja hivyo.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki kwenye maadhimisho ya kilele cha wiki ya upandaji miti Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofikia tamati leo kwa upandaji miti kwenye viwanja vya Shule ya Msingi ya Mji Mpya iliyopo Mabwepande ambapo Wilaya ya Kinondoni ilikuwa mwenyeji.

"Natoa maagizo kuwa wale wote waliopewa viwanja na serikali hapa Mabwepande ambao wameondoka viwanja vyao wanyang'anywe kwani ni wasariti na wale waliouziwa imekula kwao kwani serikali haiwatambui" alisema Sadiki.

Sadiki alitoa mwito kwa wananchi kubadilika kwa kuacha kutumia nishati ya miti na mkaa badala yake watumie gesi ambayo inapatikana kwa wingi kutokana na jitihada za serikali ili kulinda mazingira.

Aliongeza kuwa suala la upandaji miti ni endelevu hivyo kila mtu mahali alipo apande mti walau mmoja na kuitunza kwani miti ni uhai.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda alisema Manispaa hiyo inabustani kubwa  maeneo ya Kilongawima hivyo wanajipanga kuanzisha mashindano ya ukuzaji na upandaji wa miti kwa kata zake 34 na mshindi atapatiwa zawadi.

Katika hatua nyingine amesema halmshauri hiyo itawakopesha fedha wananchi waishio Mabwepande ambao waliathiriwa na mafuriko kwa ajili ya kukamilisha upatikanaji wa hati za umiliki wa viwanja vyao kabla ya mwezi wa sita badala ya kusubiri fedha kutoka ofisi ya Waziri Mkuu.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alisema changamoto ya kukamilika kwa nyumba za askari polisi na kituo cha polisi katika eneo hilo itakwisha katika kipindi kifupi kijacho.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AONGOZA UPANDAJI MITI MABWEPANDE KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA KUPANDA MITI
MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AONGOZA UPANDAJI MITI MABWEPANDE KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA KUPANDA MITI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjSWQwjw0HkYXAhOeCEWro-u-MsrlbOKtHJtzBnDWCW07-AvkNRHPQZbmFvaV3TdS1QHuE6tyfral421iI9QvRvEypPLYsBVnnhJJLf-nJD3lvJy8K81Lpe1fpICh6C7VoVd58NMH2ym6Od/s1600/SAIDI+SADIKI.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjSWQwjw0HkYXAhOeCEWro-u-MsrlbOKtHJtzBnDWCW07-AvkNRHPQZbmFvaV3TdS1QHuE6tyfral421iI9QvRvEypPLYsBVnnhJJLf-nJD3lvJy8K81Lpe1fpICh6C7VoVd58NMH2ym6Od/s72-c/SAIDI+SADIKI.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2015/04/mkuu-wa-mkoa-wa-dar-es-salaam-aongoza.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/04/mkuu-wa-mkoa-wa-dar-es-salaam-aongoza.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy