AIRTEL YAZINDUA OFA YA INTERNET BURE NCHINI

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya (katikati), ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Levi Nyakundi (k...





Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya (katikati), ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Levi Nyakundi (kushoto) na Meneja wa Kitengo cha Huduma za Intaneti wa kampuni hiyo, Gaurav Dhingra wakionyesha ishara dole wakati wa uzinduzi wa kampeni kabambe ya Airtel inayotoa ofa ya intaneti bure ijulikanayo kama ‘Na Like asubuhi’, katika hafla iliyofanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini  Dar es Salaam jana.
 
**************
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua kampeni kabambe inayotoa ofa ya internet ya BURE ijulikanayo kama “Na Like asubuhi” yenye lengo la  kuwaunganisha watanzania wote kwenye huduma ya internet na kuwawezesha kutumia na kufurahia huduma mbalimbali zinazopatikana kupitia Internet.

Ofa hii inawawezesha wateja wa Airtel kupata internet ya bure ya hadi 50MB kuanzia saaa 12 hadi saa 2 asubuhi kila siku kupitia vifaa au simu zao zenye uwezo wa kutumia huduma ya internet

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkurugenzi wa Masoko Airtel Bw, Levi Nyakundi alisema” huduma ya internet ni muhimu sana katika kuendesha na kukuza shughuli za kijamii na kiuchumi. Kadri tunavyowaunganisha watu wengi kwenye huduma hii ya internet ndivyo tunavyowezesha uchumi wetu kukua kwa kasi.  Kutokana na ripoti ya Mickinsey 2012 inayoelezea  Power of Internet inasema Intaneti
inachangia takribani asilimia 21% kukua kwa pato la dunia katika maendeleo ya kiuchumi

Airtel tunaamini kwamba maendeleo ya kukua kwa pato katika nchi zilizoendelea yanawezekana kufikia kwa haraka kupitia ongezeko la watuamiaji wa huduma ya internet.

Kwa kuliona hili, leo tunayofuraha kuzindua ofa kabambe ya “Na Like  asubuhi” itakayomuwezesha kila mtanzania kuunganishwa na huduma ya internet bila gharama yoyote  aliongeza Nyakundi

Kwa upande wake Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya alisema “Hii itasaidia wateja wa Airtel na pia itaboresha nafasi yetu ya matumizi ya intaneti duniani ambayo kwa sasa ni asilimia 17% ukilinganisha na nchi zilizoendelea’

Kwa kupitia ofa hii watu wengi zaidi wataweza kuunganishwa na mtandao na kutumia huduma za mtandao sawa na matakwa ya serikali, pia huduma za kijamii kwa njia ya mtandao zitakuwa, wakulima watapata unafuu wa kupashana habari za biashara zao, makampuni mbalimbali wataweza kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao wa intaneti aliongeza Mallya

Akiongea kuhusu kampeni hiyo Meneja wa kitengo cha huduma za internet  bw, Gaurav Dhingra alisema”masaa ya asubuhi yatakuwa yakufurahisha kupitia huduma za mtandao wa Airtel kwa sasa. Wateja wanaotumia Airtel watapata internet ya bure ya hadi 50MB kuanzia saa 12 hadi saa 2 asubuhi kila siku na kuweza kuitumia kuunganishwa na ndugu, jamaa na marafiki, kupata burdani, kupata taarifa za mambo yanayotokea duniani, kuitumia kwa shughuli za kazi na nyingnine nyingi bila kuwa na gharama zozote

Ofa hii ni rahisi, na mteja wa Airtel ataipata awapo mahali popote nchini, ukiwa na line ya Airtel iliyosajiliwa  na ikiwa una kifaa kinachokuwezesha kutumia huduma ya internet utaweza kuunganishwa moja kwa moja na  kufurahia huduma hii ya bure ya internet kuanzia saa 12 asubuhi.  Hakuna haja ya kupiga namba yoyote wala vigezo na masharti ya ziada tunachotaka kila mtanzania kufanya ni kufurahia Internet ya
BURE kutoka Airtel Aliongeza Dhingra

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: AIRTEL YAZINDUA OFA YA INTERNET BURE NCHINI
AIRTEL YAZINDUA OFA YA INTERNET BURE NCHINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg4Xndn84fvp9wOt9ph98HQZLtF-XkBzqS93hUuFv4xsCcDtSvkTOzCKtLkzZ7ifJmEDMDhV-kSqVADK9e6VRDiA6WB3A03Q8_byzlQ9MgBlspoTaBfqZTqTbfaeOoHGBori8xf9Sn3Jg7S/s1600/2.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg4Xndn84fvp9wOt9ph98HQZLtF-XkBzqS93hUuFv4xsCcDtSvkTOzCKtLkzZ7ifJmEDMDhV-kSqVADK9e6VRDiA6WB3A03Q8_byzlQ9MgBlspoTaBfqZTqTbfaeOoHGBori8xf9Sn3Jg7S/s72-c/2.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2015/04/airtel-yazindua-ofa-ya-internet-bure.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/04/airtel-yazindua-ofa-ya-internet-bure.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy