SHIRIKA LA EfG LAWAWEZESHA WANAWAKE WAJASIRIAMALI KUTOKA LUSHOTO MKOANI TANGA NA TEMEKE KUFANYA ZIARA YA MAFUNZO YA SIKU TATU KATIKA MASOKO YA MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM

  Ofisa wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Pauline Mdendemi  akizungumza na wanawake wafanyabiashara masokoni katika soko la...









 Ofisa wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Pauline Mdendemi  akizungumza na wanawake wafanyabiashara masokoni katika soko la Mchikichini Dar es Salaam jana kutoka Wilaya ya Lushoto ambao wamekuja Manispaa ya Ilala kwa mafunzo ya siku tatu  kuhusu mambo mbalimbali pamoja na masuala ya vicoba.

 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Soko la Mchikichini, Betty Mtewele (katika), akizungumza na wanawake wajasiriamali.
 Katibu wa Umoja wa Wanawake Soko la  Mchikichini, Juliana Richard akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
 Mjasiriamali kutoka Lushoto Tanga, Magreth Mkomwa (katikati), akiuliza swali katika mafunzo hayo.
 Wanawake wajasiriamali wakiwa kwenye mafunzo hayo.
 Wanawake wajasiriamali wakiwa kwenye mafunzo hayo.
 Mwenyekiti wa Soko la Lukozi lililopo wilayani Lushoto, Zakati Tendwa akichangia jambo.
 Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja.
 Wajasiriamali hao wakitembelea soko la Mchikichini kuona kazi za wenzao zinauzwa katika soko hilo.
 Hapa wakiangalia nguo aina ya batiki zinazotengenezwa na wenzao wa soko hilo.
Hapa wakifurahia gauni la batiki katika soko hilo.

Dotto Mwaibale

WANAWAKE wafanyabiashara katika masoko wametakiwa kujenga tabia ya kutunza kumbukumbu zao na kufanya vikao vya mara kwa mara jambo litakalosaidia kuwapunguzia changamoto za kazi zao.

Mwito huo ulitolewa na Ofisa wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Pauline Mdendemi wakati akizungumza na wanawake wafanyabiashara masokoni Dar es Salaam jana kutoka Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga na Manispaa ya Temeke ambao wapo  Manispaa ya Ilala kwa ziara ya siku tatu ya mafunzo mbalimbali pamoja na masuala ya vicoba  yaliyofikia tamati jana. 

"Jengeni tabia ya kutunza kumbukumbu zetu pamoja na kufanya vikao vya mara kwa mara itawasaidia kujua changamoto mlizonazo na kuzitatua " alisema Mdendemi.

Mdendemi alisema shirika hilo la EfG limefanikiwa kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa programu ya "Sauti ya Mwanamke Sokoni" kwa Manispaa ya Ilala ambapo wanawake wajasiriamali   wameweza kupaza sauti ya kupinga vitendo vya kinyanyasaji dhidi yao.


Alisema shirika hilo lilifanya mradi wa miaka mitatu katika manispaa hiyo ambayo sasa imekuwa ya mfano na ndio maana wafanyabiashara wanawake kutoka Lushoto mkoani Tanga wamefika kujifunza ili nao elimu hiyo waipeleke kwa wenzao.

Alisema lengo la mafunzo ni kuwapa fursa washiriki hao kuweza kujifunza kutoka kwa wanawake wajasiriamali sokoni katika manispaa ya Ilala masuala mbalimbali ikiwemo mbinu za kufanya ushawishi na utetezi ili kuboresha mazingira ya ufanyaji kazi katika masoko.

Alitaja malengo mengine kuwa ni namna ya kuongeza wanachama wa umoja na vicoba, uendeshaji vikao vya umoja sokoni na namna mfumo wa kuweka na kukopa (Vicoba) unavyoweza kuwasaidia wanawake wajasiriamali kukuza vipato vyao na kuboresha biashara na maisha yao kwa ujumla.

Mdendemi alitaja wajasiriamali walionufaika na mafunzo hayo kuwa ni wanawake wanne kutoka wilaya ya Lushoto, Lukozi Lushoto watatu, Chamazi watatu na Temeke Sterio watatu.

Mwenyekiti wa soko la Lukozi kutoka Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, Zakati Tendwa alisema mafunzo hayo yamewafumbua macho kwani walikkuwa hawajui chochote kuhusu masuala ya vicoba na kwa niaba ya wenzake amelishukuru shirika la EfG kwa kuwapigania wanawake wajasiriamali masokoni. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)






COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SHIRIKA LA EfG LAWAWEZESHA WANAWAKE WAJASIRIAMALI KUTOKA LUSHOTO MKOANI TANGA NA TEMEKE KUFANYA ZIARA YA MAFUNZO YA SIKU TATU KATIKA MASOKO YA MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM
SHIRIKA LA EfG LAWAWEZESHA WANAWAKE WAJASIRIAMALI KUTOKA LUSHOTO MKOANI TANGA NA TEMEKE KUFANYA ZIARA YA MAFUNZO YA SIKU TATU KATIKA MASOKO YA MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjjpDYcEUUGfXCFic0ivcg6OVeEANh3pHvBv3-ZoVOgnfsXp7BHUrWsL28EzsnP9nP2pWPqnn3ZY2WD-fLbCtvuoidg57qY80OCB2a3a4R5iw9zhs3jTab4U9OzRbgKRlgg16FsshWfrvU/s1600/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjjpDYcEUUGfXCFic0ivcg6OVeEANh3pHvBv3-ZoVOgnfsXp7BHUrWsL28EzsnP9nP2pWPqnn3ZY2WD-fLbCtvuoidg57qY80OCB2a3a4R5iw9zhs3jTab4U9OzRbgKRlgg16FsshWfrvU/s72-c/1.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2015/03/shirika-la-efg-lawawezesha-wanawake.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/03/shirika-la-efg-lawawezesha-wanawake.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy