RAIS KAGAME WA RWANDA AWASILI DAR NA KUHUDHURIA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA KANDA YA KATI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akisalimiana na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kag...




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akisalimiana na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Kagame yupo nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Ukanda wa Kati kuhusu Uwekezaji na Viwanda unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Rais Kagame akipokea shada la maua kutoka kwa mtoto Elizabeth Jackson kama ishara ya kumkaribisha nchini Tanzania. 
Rais Kagame akipokea kwa heshima alipowasili uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam leo.
Rais Kagame na Waziri Membe wakiangalia burudani ya ngoma za asili uwanjani hapo. 

Waziri Membe akiwa ameongozana na Rais Kagame mara baada ya kuburudika na ngoma za asili. (Picha na Reginald Philip)


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Kanda ya Kati (Central Corridor Conference) ulioanza jana na kumalizika leo Machi 26, 2015.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Kanda ya Kati (Central Corridor Conference) ulioanza jana na kumalizika leo Machi 26, 2015.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wageni wake Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Pierre Nkurunzinza kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Kanda ya Kati (Central Corridor Conference) ulioanza jana na kumalizika leo Machi 26, 2015.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakiwa kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Kanda ya Kati (Central Corridor Conference) ulioanza jana na kumalizika leo Machi 26, 2015.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakiwa kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Kanda ya Kati (Central Corridor Conference) ulioanza jana na kumalizika leo Machi 26, 2015.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Paul Kagame wa Rwanda katika picha ya pamoja na mawaziri wa Tanzania, Kenya, DRC na Uganda kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Kanda ya Kati (Central Corridor Conference) ulioanza jana na kumalizika leo Machi 26, 2015.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  Rais Paul Kagame wa Rwanda wakisiliza maelezo toka kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Rished Bade walipotembelea kituo cha kulipia ushuru wa aina zote chini ya paa moja  katika bandari ya Dar es Salaam leo Machi 26, 2015.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  Rais Paul Kagame wa Rwanda wakisiliza maelezo toka kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Rished Bade walipotembelea kituo cha kulipia ushuru wa aina zote chini ya paa moja  katika bandari ya Dar es Salaam leo Machi 26, 2015.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  Rais Paul Kagame wa Rwanda wakiteta jambo walipotembelea  bandari ya Dar es Salaam leo Machi 26, 2015.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  Rais Paul Kagame wa Rwanda wakiteta jambo walipotembelea  bandari ya Dar es Salaam leo Machi 26, 2015.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  Rais Paul Kagame wa Rwanda wakiteta jambo walipotembelea  bandari ya Dar es Salaam leo Machi 26, 2015.

Rais Paul Kagame wa Rwanda akipeperusha bendera kuashiria kuzinduliwa kwa safari za treni za mizigo kuelekea Rwanda katika stesheni ya reli ya Dar es Salaam akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho kikwete leo Machi 26, 2015.
(PICHA NA IKULU)
 *****************



THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425


Coat of Arms
PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake, Rais Paul Kagame wa Rwanda, leo, Alhamisi, Machi 26, 2015, wametembelea Bandari ya Dar es Salaam na baadaye Rais Kagame ameanzisha safari ya treni maalum za kusafirisha mizigo ya Rwanda kutoka Tanzania.
Rais Kagame amewasili nchini asubuhi ya leo na kufungua Mkutano wa Wawekezaji katikaUjenzi wa Miundombinu Ukanda wa Kati (High Level Investors Forum – Central Corridor Development Acceleration Programme) uliofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere mjini Dar es Salaam.
Mara baada ya hotuba ya ufunguzi na kipindi cha maswali kutoka kwa washiriki na majibu kutoka kwa viongozi wa nchi tano zinazounda Shirika la Uwezeshaji wa Usafiri wa Ukanda wa Kati (The Central Corridor Transit Transport Facilitation Agency (CCTTFA), viongozi hao wawili wamekwenda Bandari ya Dar es Salaam.
CCTTFA lilianzishwa Septemba 2, mwaka 2006, na Makubaliano yaliyotiwa saini na nchi tano ambazo zinanufaika na usafiri wa Ukanda wa Kati – Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Rwanda na Uganda.
Katika Bandari ya Dar es Salaam, Rais Kagame na mwenyeji wake wameanza kwa kutembelea ofisi mpya za Mpango wa Ukusanyaji Ushuru kwa Pamoja (Single Customs Territory) miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), mpango ulioanza kutumika Julai mwaka jana, 2014. Chini ya Mpango huo, kila nchi inashughulikia mizigo yake yenyewe, ikiwa ni pamoja na kukusanya kodi yake.
Rais Kagame na mwenyeji wake wametembelea ofisi za Mamlaka ya Kodi ya Rwanda (RRA) na Mamlaka ya Kodi ya DRC ambako walipewa maelezo kuhusu faida za mpango huo.
Miongoni mwa mambo mengine, marais hao walielezwa kuwa chini ya Mpango huo, waagizaji wa mizigo ya Rwanda, kupitia Bandari ya Dar es Salaam, sasa wanajaza fomu moja tu badala ya tatu na sasa mizigo ya Rwanda inachukua siku mbili tu kutoka Bandari ya Dar es Salaam hadi Kigali, badala ya siku kati ya tano na 10 kabla ya kuanzishwa Mpango huo.
Nchi ambazo tayari zimefungua ofisi zao katika Bandari hiyo kutekeleza Mpango huo ni Tanzania yenyewe, Burundi, DRC na Rwanda. Uganda inakamilisha maandalizi ya utekelezaji na Zambia imeonyesha nia ya kujiunga na Mpango huo, kwa sababu inapitishia mizigo yake katika Bandari ya Dar es Salaam, hata kama siyo mwanachama wa EAC.
Kutoka kwa ofisi za Single Customs Territory, viongozi hao wamekwenda kwenye Bandari ya Dar es Salaam ambako wamepatiwa maelezo kuhusu jinsi utendaji wa Bandari hiyo ulivyoboreka katika miaka miwili iliyopita.
Aidha, viongozi hao wameelezwa jinsi gani pia utendaji wa kampuni binafsi ya upakiaji na upakuaji mizigo ya TICTS inavyofanya kazi na ilivyoboresha utendaji wake katika sehemu nne za meli kutia nanga (berths) ambako inafanyia kazi yake katika Bandari hiyo yenye sehemu 11 za kupakia na kupakulia mizigo.
Katika Bandari hiyo, marais hao wameelezwa kuwa katika miaka mitano iliyopita, kiwango cha mizigo inayopitia katika Bandari hiyo kimekuwa kinaongezeka kwa wastani wa asilimia 12.8 kila mwaka.
Wameelezwa pia kuwa mwaka jana, kiasi cha tani milioni 14.6 ya mizigo kilipitia katika Bandari hiyo zikiwemo kontena 621,000 na kuwa kati ya mizigo hiyo kiasi cha asilimia 34, sawa na mizigo tani milioni 5.020 ilikuwa mizigo kwa ajili ya nchi za jirani.
Aidha, viongozi hao wameelezwa kuwa muda wa kontena kukaa Bandarini hapo sasa ni siku tisa tu badala ya siku 21 Februari mwaka 2008, muda wa meli kukaa nje ya Bandari ikisubiri kuingia Bandarini ili ipakuliwe, sasa ni siku moja unusu badala ya siku tatu unusu za mwaka 2013.
Marais Kagame na Kikwete pia wameelezwa kuwa usalama wa mizigo ya waagizaji sasa umeongezeka mno, kiasi cha kwamba halijakuwepo tukio hata moja la wizi wa mizigo ya wateja yakiwemo magari na spea zake kwa miaka mitatu mfululizo sasa.
Bandari ya Dar es Salaam ambayo huhudumia mizigo ya nchi saba – ya Tanzania yenyewe, Malawi, Zambia, DRC, Burundi, Rwanda na Uganda pia huendesha Bandari kwenye maziwa makuu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa.
Jana, Jumatano, Machi 25, 2015, Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi pamoja na wawakilishi wa nchi za DRC na Uganda pia walianzisha safari za treni za namna hiyo kwenda katika nchi zao.
Rais Kagame ameondoka nchini kurejea kwao leo baada ya kuanzisha safari hizo na mkutano wenyewe kuhusu Ukanda wa Kati, ambao pia ulihudhuriwa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, umemalizika jioni ya leo.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
26 Machi, 2015
















COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS KAGAME WA RWANDA AWASILI DAR NA KUHUDHURIA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA KANDA YA KATI JIJINI DAR ES SALAAM LEO
RAIS KAGAME WA RWANDA AWASILI DAR NA KUHUDHURIA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA KANDA YA KATI JIJINI DAR ES SALAAM LEO
http://4.bp.blogspot.com/-iVheZrGK4uc/VRQWxq61jQI/AAAAAAADRig/3FNBvGj9apU/s1600/IMG_5868.JPG
http://4.bp.blogspot.com/-iVheZrGK4uc/VRQWxq61jQI/AAAAAAADRig/3FNBvGj9apU/s72-c/IMG_5868.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2015/03/rais-kagame-wa-rwanda-awasili-dar-na.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/03/rais-kagame-wa-rwanda-awasili-dar-na.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy