Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kijeshi mjini Riyadh...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kijeshi mjini Riyadh, Saudi
Arabia, asubuhi ya Januari 25 Jumapili, Januari 25, kuhani kifo cha
Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa
Ijumaa ya wiki iliyopita. Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah,
Rais Kikwete ataendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi. (PICHA NA IKULU)
**************
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akiwasili mjini Riyadh, Saudi Arabia,asubuhi ya Jumapili, Januari 25,
2015, kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki
Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita.
Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah, Rais
Kikwete ataendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa
ziara za kikazi.
Mjini Berlin, Ujerumani ambako Rais Kikwete
alitarajiwa kuwasili Jumatatu, Januari 26, akitokea Riyadh, Saudi Arabia,
anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Global Alliance for Vaccines and
Immunization (Gavi Alliance) ambako viongozi mbalimbali duniani watajadili
jinsi ya kuboresha mipango ya utoaji chanjo kwa watoto wadogo hasa katika nchi
zinazoendelea.
Baada ya kumaliza ziara yake Ujerumani, Rais
Kikwete atakwenda Ufaransa ambako miongoni mwa mambo mengine atakutana na
kufanya mazungumzo na viongozi wa Ufaransa.
Aidha, Rais Kikwete atafungua jengo jipya la
Ubalozi wa Tanzania katika Ufaransa na pia nyumba ya balozi.
Rais Kikwete baada ya kumaliza ziara zake za
kikazi katika Ujerumani na Ufaransa atakwenda Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria
Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
– Dar es Salaam.
25 Januari, 2015
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah, Rais Kikwete ataendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi.
Mjini Berlin, Ujerumani ambako Rais Kikwete alitarajiwa kuwasili Jumatatu, Januari 26, akitokea Riyadh, Saudi Arabia, anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Global Alliance for Vaccines and Immunization (Gavi Alliance) ambako viongozi mbalimbali duniani watajadili jinsi ya kuboresha mipango ya utoaji chanjo kwa watoto wadogo hasa katika nchi zinazoendelea.
Baada ya kumaliza ziara yake Ujerumani, Rais Kikwete atakwenda Ufaransa ambako miongoni mwa mambo mengine atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Ufaransa.
Aidha, Rais Kikwete atafungua jengo jipya la Ubalozi wa Tanzania katika Ufaransa na pia nyumba ya balozi.
Rais Kikwete baada ya kumaliza ziara zake za kikazi katika Ujerumani na Ufaransa atakwenda Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).
COMMENTS