BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA AFANYA ZIARA MKOANI KAGERA KUKAGUA ENEO LA KUJENGA CHUO CHA KISASA CHA UFUNDI (VETA) NA KUONA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA MKOA

Balozi wa China nchini Tanzania,LU Youqing akicheza ngoma ya asili ya Mkoa wa Kagera wakati alipokuwa akilakiwa kwenye uwanja wa...



Balozi wa China nchini Tanzania,LU Youqing akicheza ngoma ya asili ya Mkoa wa Kagera wakati alipokuwa akilakiwa kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella .
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella akimkabidhi Balozi wa China nchini Tanzania,LU Youqing Hati na ramani eneo lililotengwa na serikali ya mkoa kwa ajili ya kujenga chuo cha Ufundi (VETA) cha Kitaifa kilichoahidiwa na serikali ya China wakati wa ziara ya Rais Kikwete nchini humo mwaka jana. 
Balozi wa China nchini Tanzania,LU Youqing akipokea zawadi ya ramani ya Afrika Mashari iliyochorwa kutoka kwa wanafunzi wa shule ya Mgeza Mseto.
Balozi LU akisaini kitabu cha wageni Bukoba airport.
Balozi wa China nchini Tanzania,LU Youqing akitoa zawadi kwa wanafunzi.
Picha ya Pamoja.

Balozi wa China nchini Tanzania,LU Youqing yupo mkoani Kagera  kwa ziara ya siku mbili kukagua eneo  lililotengwa na serikali ya mkoa kwa ajili ya kujenga chuo cha Ufundi (VETA) cha Kitaifa kilichohaidiwa na serikali ya China wakati wa ziara ya Rais Kikwete nchini humo mwaka jana Oktoba 2014.

Akimkaribisha mkoani Kagera Mkuu wa Mkoa John Mongella alimweleza Balozi LU kuwa mkoa wa Kagera una fursa nyingi za uwekezaji ambazo ni pamoja na uwekezaji katika viwanda vidogo vidogo vya kusindika bidhaa mbalimbali ili kuinua uchumi wa wananchi na mkoa kwa ujumla.

Bw. Mongella alimwomba Balozi LU kufikiria kuleta wataalamu wa afya hasa madaktari kutoka nchini mwake hususani katika hospitali ya Rufaa ya mkoa ili kutoa huduma kwani mkoa upo mbali sana na hospitali za Rufaa za taifa jambo ambalo huleta usumbufu kwa wagojwa wanaohitaji huduma za hospitali za rufaa.

Balozi LU katika kutoa salaamu zake alisema kuwa  amefurahi kufika mkoani Kagera kwa mara ya pili na akasifu mkoa kwa kuwa na hali nzuri ya hewa na kubarikiwa katika nyanja mbalimbali za kiuchumi. Aidha, alisema kutokana na urafiki wa nchi mbili za Tanzania na China amefurahi kuwa sasa kutakuwa na alama ya urafiki huo katika mkoa wa Kagera.

Pamoja na kuusifia Mkoa wa Kagera imeisifia serikali ya Tanzania kwa kutekeleza miradi ya maendeleo,alisema kuwa  ukipita mikoani unaona mabadiliko makubwa kuliko ilivyokuwa hapo nyuma.  Ambapo alisema kuwa serikali ya China imewekeza na kutekeleza miradi ya maendeleo nchini Tanzania yenye thamani ya bilioni 3.15  dolla za kimarekani  kwa mwaka  2013/2014.

Balozi LU alitembelea kiwanja cha hekta 26,000 kilichopo eneo la Kahororo katika Halamashauri ya Manispaa ya Bukoba ambapo chuo cha ufundi (VETA) kitajengwa na kujionea mwenyewe kitakapojengwa chuo hicho. Pia alitembelea shule ya Mgeza Mseto ambako aliwahi kutembelea na kutoa msaada wa komputa ili kuona wanafunzi wa shule hiyo maendeleo yao.

Katika shule ya msingi Mgeza Mseto yenye wanafunzi wa bweni na kutwa pia inapokea watoto wa aina tatu, watoto wenye albinisimu, watoto wenye ulemavu wa viungo, na watoto wa kawaida,  Balozi LU alisema amefurahi kuwaona tena na kuhaidi kutoa msaada zaidi wa komputa ili watoto waweze kila mmoja kujifunza komputa.

Katika maelezo yake Balozi LU aliufananisha mkoa wa Kagera na Jimbo la Chandog la nchini China na kusema kuwa atahakikisha unaungaisha urafiki kati ya mkoa wa Kagera na jimbo hilo ili kuleta maendeleo zaidi Kagera. Vilevile alisema atahakikisha anfanya mpango wa Tanzania hasa mkoa wa Kagera unakuwa na utaratibu wa kubadilishana walimu kutoka nchini China.

Maeneo ya uwekezaji ambayo mkoa umeyatenga kwa ajili ya uwekezaji ni pamoja na Kilimo cha kisasa katika maeneo mbalimbali, Ufugaji wa kisasa wa samaki, Ujenzi wa bandari ya Kemondo(contena terminal)  na ufugaji wa kisasa wa nyuki pamoja na ujenzi wa chuo cha ufundi (VETA)
(Imeandaliwa na Glob ya Jamii)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA AFANYA ZIARA MKOANI KAGERA KUKAGUA ENEO LA KUJENGA CHUO CHA KISASA CHA UFUNDI (VETA) NA KUONA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA MKOA
BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA AFANYA ZIARA MKOANI KAGERA KUKAGUA ENEO LA KUJENGA CHUO CHA KISASA CHA UFUNDI (VETA) NA KUONA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA MKOA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh9mkKb9wVjk3-_H3DUgxj9TxpcOdGbBhm23NyVTp-KUJxyQD3ndhDwSH58ZFxnxXOAXwhWNpxg8Kl8nHG10jBheIa4GxnnquDwbLo3eQMFWMYCdkAYd10AvLkmfRdQjz27QjE0ajyBqok/s1600/Balozi+LU+akicheza+nngoma+uwanja+wa+ndege+mara+baada+ya+kuwasili.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh9mkKb9wVjk3-_H3DUgxj9TxpcOdGbBhm23NyVTp-KUJxyQD3ndhDwSH58ZFxnxXOAXwhWNpxg8Kl8nHG10jBheIa4GxnnquDwbLo3eQMFWMYCdkAYd10AvLkmfRdQjz27QjE0ajyBqok/s72-c/Balozi+LU+akicheza+nngoma+uwanja+wa+ndege+mara+baada+ya+kuwasili.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2015/01/balozi-wa-china-nchini-tanzania-afanya.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/01/balozi-wa-china-nchini-tanzania-afanya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy