MAHAFALI YA 44 YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM KATIKA PICHA

Kiongozi wa kwaya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Daktari Kedmon Mapana akihitimisha wimbo kwa mtindo wake baada ya kutoa burudani kati...


Kiongozi wa kwaya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Daktari Kedmon Mapana akihitimisha wimbo kwa mtindo wake baada ya kutoa burudani katika mahafali ya 44 ya UDSM yaliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam Novemba 8 2014.
BAADHI ya wahitimu katika fani mbalimbali wakiimba wimbo wa taifa wakati wa kuanza mahafali ya 44 ya chuo Kikuu cha Dar es Salam (UDSM) yaliyofanyika ukumbubi wa Mlimani City jijini humo mwishoni mwa wiki.

Sehemu ya wahitimu katika fani mbalimbali wakiwa katika mahafali ya 44 ya chuo Kikuu cha Dar es Salam (UDSM) wakifuatilia matukio mwishoni mwa wiki.

BAADHI ya Madkatari wa fani mbalimbali wakiwa katika mahafali ya 44 yaliyofanyika ukumbi wa Mlimani city Dar es Salam (UDSM) mwishoni mwa wiki.

BAADHI ya Madkatari wa fani mbalimbali wakiwa katika mahafali ya 44 baada kuhitimu mwishoni mwa wiki.







Mdau Daktari Misanya Bingi (katikati) akiwa na watunukiwa wengine baada ya kutunukiwa Digrii ya Udaktari wa Falsafa, katika mahafali hayo.

Mjane wa aliyekuwa Mkuu wa UDSM, Celestine Muombeki Kazaura, marehemu Balozi Fulgence Michael Kazura akienda kusoma hotuba baada ya kupokea Digrii ya Heshima ya Udaktari wa Sayansi (Doctor of Science Honoris Causa), kwa niaba mumewe baada ya kutunukiwa wakati wa mahafali hayo.


  Lord David John Sainsbury akifuatilia matukio kabla ya kutunukiwa Digrii ya Heshima ya Udaktari wa Sayansi (Doctor of Science Honoris Causa), wakati wa mahafali hayo. Kulia ni Mjane wa aliyekuwa Mkuu wa UDSM, Celestine Muombeki Kazaura, Balozi Fulgence Michael Kazura. 

Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Balozi Nicholas A. Kuhanga Digrii ya Heshima ya Udaktari wa Sayansi (Doctor of Science Honoris Causa), Lord David John Sainsbury wakati wa mahafali hayo. Kushoto ni Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala.  

Kiongozi wa kwaya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Daktari Kedmon Mapana akiwaongoza wanakwaya wenza kutoa burudani katika mahafali hayo.

Kiongozi wa kwaya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Daktari Kedmon Mapana akihitimisha wimbo kwa mtindo wake baada ya kutoa burudani katika mahafali hayo.

Wadau mabalimbali wakiwa katika mahafali hayo.

Bendi ya JWTZ ikitoa burudani wakati wa mahafali hayo.

Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Balozi Nicholas A. Kuhanga akimtunuku Digrii ya Udaktari wa Falsafa, mmoja wa wahitimu katika mahafali hayo.

Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Balozi Nicholas A. Kuhanga akimtunuku Digrii ya Udaktari wa Falsafa, Shiundu Barasa wakati wa mahafali ya 44 mwishoni mwa wiki.

BAADHI ya Madaktari wa fani mbalimbali wakiwa katika mahafali ya 44 baada kuhitimu mwishoni mwa wiki.

BAADHI ya Madaktari wa fani mbalimbali wakiwa katika mahafali ya 44 baada kuhitimu mwishoni mwa wiki.


BAADHI ya wahitimu katika fani mbalimbali wakiwa katika mahafali ya 44 ya chuo Kikuu cha Dar es Salam (UDSM) mwishoni mwa wiki. (Imeandaliwa na Robert Okanda)
****************************
UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
P.O. BOX 35091  DAR ES SALAAM  TANZANIA
Press Release
Direct: +255 22 2410751 Telegraphic Address: UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
Telephone: +255 22 2410500-8 ext. 2473/2009 E-mail: relation@admin.udsm.ac.tz
Telefax: +255 22 2410078 Website address: www.udsm.ac.tz
MAHAFALI YA 44 YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kampasi ya Mwalimu Julius Nyerere Mlimani kinapenda kuwataarifu wadau wa Chuo na umma kwa ujumla kuwa kinafanya Mahafali ya Arobaini na Nne (44) mwezi Novemba 2014. Mahafali haya yamegawanyika katika makundi mawili. Kundi la kwanza, litakalofanya mahafali yake tarehe 8 Novemba 2014, litatunuku Shahada za Uzamivu, Umahiri, na Stashahada za Uzamili, pamoja na shahada za awali kwa wahitimu wa Chuo cha Uhandisi na Teknolojia, Chuo cha Sayansi Asilia na Tumizi, na Chuo cha Habari na Teknolojia za Mawasiliano. Kundi la pili litafanya mahafali tarehe 15 Novemba 2014; hili litawahusu wahitimu wa shahada za awali zilizobakia, yaani kutoka Chuo cha Sayansi za jamii, Chuo cha Fani za Binadamu, Shule Kuu ya Elimu, Shule Kuu ya Masomo ya Biashara, Shule Kuu ya Sheria, Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma, Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, na kilichokuwa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ardhi na Usanifu Majengo (UCLAS).
Mwaka huu 2014, jumla ya wahitimu 953 wamefuzu masomo ya uzamili, kama ifuatavyo. Shahada za Uzamivu: 63 (wanaume 43, wanawake 20); Shahada za Umahiri: 800 (wanaume 490, wanawake 310); Stashahada za Uzamili: 90 (wanaume 55, wanawake 35). Kwa upande wa Shahada za Awali, idadi ya wahitimu imeongezeka kutoka 4,209 mwaka 2013 hadi 5,745 mwaka 2014, ambayo ni sawa na asilimia 36. Uwiano wa jinsia kati ya wahitimu wetu umeendelea kuboreka. Idadi ya wanawake wahitimu imeongezeka kutoka asilimia 37 (2013) hadi asilimia 40 kwa Shahada za Awali, na kutoka asilimia 34 (2013) hadi 37 kwa wahitimu wa shahada za uzamili.
Mchanganuo wa wahitimu kwa tuzo kwa mwaka 2014 ukilinganishwa na mwaka 2013
Na.
Tuzo
2014
2013
wanaume
wanawake
Jumla
1.
Shahada ya Uzamivu (PhD)
43
20
63
42
2.
Shahada ya Umahiri (Master)
490
310
800
1,065
3.
Stashahada ya Uzamili (Postgraduate)
55
35
90
167
4.
Shahada ya Awali (Bachelor)
3,423
2,322
5,745
4,209 JUMLA 4,011 2,687 6,698 5,731
Kutokana na ongezeko la wahitimu, uongozi na wadau wa Chuo wanaendelea kutafakari mbinu na mikakati bora zaidi kuhusu uwezekano wa kuongeza idadi ya makundi ya mahafali
kutoka mawili yaliyopo, ili mahafali yafanyike kwa makundi madogo zaidi; moja ya mbinu zinazofikiriwa ni kutenganisha kundi la shahada za uzamili na makundi ya shahada za awali.
Aidha kwa namna ya pekee katika awamu ya kwanza ya Mahafali haya, tarehe 8 Novemba 2014, Mkuu wa Chuo atatunuku shahada za heshima kwa watu wawili mashuhuri. Wa kwanza ni Hayati Balozi Fulgence Michael Kazaura (1940–2014) ambaye atatunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari katika Fasihi (honoris causa). Hayati Kazaura anatunukiwa shahada hii kwa sababu ya mchango wake mkubwa alioutoa kwa maendelea ya Chuo hiki na taifa kwa ujumla, wakati wa uhai wake. Alitoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya Chuo, na hasa katika mageuzi ya mfumo wa uongozi, utawala na taaluma tangu mwaka 1993 hadi mwisho wa uhai wake 2014. Shahada ya Juu ya Heshima ya marehemu Balozi Kazaura itapokewa na mke wake Bibi Celestina Mwombeki Kazaura kwa niaba ya marehemu.
Wa pili ni Lord David John Sainsbury ambaye atatunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari katika Sayansi (honoris causa). Mheshimiwa Sainsbury ni msomi mbobezi aliyejipambanua katika sura mbalimbali za umahiri, kama vile mwanasiasa, mjasiriamali, kiongozi, mtawala na mwandishi. Amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi na za kisiasa nchini Uingereza. Amejihusisha na harakati za kuondoa umaskini nchini Tanzania tangu mwaka 1992 kupitia shirika la Tanzania Gatsby Trust, ambalo limekuwa na uhusiano wa karibu na Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (CoET) cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuweza kuanzisha shahada kadhaa za awali na udhamini wa wanafunzi katika shahada za Umahili.
Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unawakaribisha wadau wote wa elimu kushiriki nasi katika mahafali haya ya 44. Mwisho, tunamhamasisha kila mhitimu kwenda kulitumikia Taifa kwa moyo wote kwa njia ya kujiajiri, kuajiri au kuajiriwa na hatimaye kuwa balozi mwema wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Imetolewa na
Prof. Rwekaza S. Mukandala
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAHAFALI YA 44 YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM KATIKA PICHA
MAHAFALI YA 44 YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM KATIKA PICHA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjeVNTlJ0u_XHKJt3sOGaSaFdtK_5GLmy1_kVhhNn7c_YEIJ4F7Dj12nOvovP8jjwfjOwkNQbSdDOTbqECKb5OHXbEt6dld5JjOmmCqmKCLz5wY3V5SBrhyphenhyphenPlb-EG4kEQJpZ8mhQU_ej6cy/s1600/G14.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjeVNTlJ0u_XHKJt3sOGaSaFdtK_5GLmy1_kVhhNn7c_YEIJ4F7Dj12nOvovP8jjwfjOwkNQbSdDOTbqECKb5OHXbEt6dld5JjOmmCqmKCLz5wY3V5SBrhyphenhyphenPlb-EG4kEQJpZ8mhQU_ej6cy/s72-c/G14.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2014/11/mahafali-ya-44-ya-chuo-kikuu-cha-dar-es.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2014/11/mahafali-ya-44-ya-chuo-kikuu-cha-dar-es.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy