RAIS KIKWETE AKUTANA NA MEYA WA MJI WA VALLEJO WA MAREKANI, AMKARIBISHA KATIBU MKUU, DK SEZIBERA NA APOKEA TAARIFA YA VIONGOZI WA AF...
RAIS KIKWETE AKUTANA NA MEYA WA MJI WA VALLEJO WA MAREKANI, AMKARIBISHA KATIBU MKUU, DK SEZIBERA NA APOKEA TAARIFA YA VIONGOZI WA AFRIKA IKULU DAR ES SALAAM
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Meya wa Mji wa Vallejo
nchini Marekani Mstahiki Osby Davis alipomtembelea Ikulu jijini Dar
es salaam leo. Meya Davis yuko nchini na ujumbe wa
wafanyabiashara 15 kutoka Vallejo wakiwa katika ziara ya kutafuta fursa za
uwekezaji na ushirikiano. Mji wa Vallejo ni mji dada na wa Bagamoyo katika mkoa
wa Pwani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akifurahia jambo na Meya wa Mji wa
Vallejo nchini Marekani Mstahiki Osby Davis alipomtembelea Ikulu
jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akipokea zawadi ya sanamu ndogo ya mji wa Vallejo toka kwa Meya wa Mji wa
Vallejo nchini Marekani Mstahiki Osby Davis alipomtembelea Ikulu
jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiwa katika picha na Meya wa Mji wa Vallejo nchini Marekani Mstahiki
Osby Davis na ujumbe wake walipomtembelea Ikulu jijini Dar es
salaam leo. Meya Davis yuko nchini na ujumbe wa
wafanyabiashara 15 kutoka Vallejo wakiwa katika ziara ya kutafuta fursa za
uwekezaji na ushirikiano.
Rais
Dk Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa jumuiya
ya Afrika Mashariki Dk Richard Sezibera ikulu jijini Dar es Salaam jana. (Picha
na Freddy Maro)
|
Rais
Dk Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Katibu Mkuu wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki Dk Richard Sezibera.
|
COMMENTS