FUJO KILA KONA Magari Nyumba Pikipiki zachomwa moto

          Nyumba ikiteketea kwa moto huko masasi Baadhi ya magari  yalio chomwa Moto na  wananchi               Vijan...

Click image for larger version. 

Name: Elimu.jpg 
Views: 0 
Size: 1.10 MB 
ID: 80944
          Nyumba ikiteketea kwa moto huko masasi
Click image for larger version. 

Name: Magari.jpg 
Views: 0 
Size: 1.22 MB 
ID: 80947
Baadhi ya magari  yalio chomwa Moto na  wananchi
Click image for larger version. 

Name: Ambulance.jpg 
Views: 0 
Size: 1.24 MB 
ID: 80948

Click image for larger version. 

Name: Genereta.jpg 
Views: 0 
Size: 1.50 MB 
ID: 80945

          


Vijana wakazi wa Dumila na vitongo vyake wakiangusha gari aina ya Land Cruizer T 241 AMS mali ya mfugaji katika barabara kuu ya Dodoma-Morogoro wakati wa vurugu zilizodumu kwa masaa sita kwa kuweka vizuwizi kwa lengo la kumshinikiza mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bebdera kusikiliza kero za wakulima. (Picha na Juma Mtanda)


MAENEO ya mikoa ya Morogoro, Mtwara na Dar es Salaam, jana yaligeuka uwanja wa fujo na vurugu zilizosababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali, huku polisi wakitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi.
Vurugu hizo zimehusisha wakulima na wafugaji wa jamii ya Kimasai kwa upande mmoja wa Morogoro, Mtwara Mikindani wananchi waliizingira nyumba ya Diwani wa Kata ya Mikindani kwa madai ya kuwahifadhi watu wanaodaiwa kuwa washirikina ndani ya nyumba yake, huku Dar es Salaam eneo la Kariakoo, polisi na Wamachinga wakipambamba na Mgambo wa Jiji.
Mkoani Mororgoro mtu mmoja aliyefahamiwa kwa jina la Mohamed Msigara (60) amefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kutokea vurugu kati ya wakulima na wafugaji Kijiji cha Dumila, wila yani Kilosa, baada ya wafugaji wa Jamii ya Kimasai kuingiza mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima yaliyo katika Kitongoji cha Mfulu, Kilosa.
Pamoja na mauaji hayo, wasafiri waliokuwa wakitumia Barabara ya Morogoro – Dodoma, nao walionja machungu ya vurugu hizo, baada ya kukwama kwa saa 5 kutokana na wananchi wa kijiji hicho, kufunga barabara kwa mawe, magogo ya miti na kuchoma magurudumu ya gari.
Wananchi hao walichukua hatua hiyo huku wakisisitiza kutaka kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, ili kumaliza mvutano huo.
Katika vurugu hizo wanakijiji hao walivunja vioo vya madirisha ya baadhi ya nyumba tano za kulala wageni, kuharibu gari dogo aina ya Landcruser pamoja na kupora mali mbalimbali zi nazodaiwa kumilikiwa na wafanyabiashara wa jamii ya Kimasai.
Kabla ya kufanya uharibifu huo saa 2:30 asubuhi, wananchi hao walifanya maandamano sambamba na kusimama katikati ya barabara, hali iliyosababisha polisi kufika eneo hilo kwa ajili ya kuwadhibiti.
Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU), walifika eneo la tukio 5:20 asubuhi na kufanikiwa kuwatawanya wananchi hao kwa kutumia mabomu ya machozi, hatimaye kufungua barabara hiyo.
Pamoja na barabara hiyo ya Morogoro – Dodoma, wananchi hao pia walifunga barabara ya Dumila- Kilosa, hivyo kuyafanya magari yaliyokuwa yakitumia barabara hiyo kukwama kwa zaidi ya saa sita na kusababisha usumbufu kwa wasafiri waliokuwa wakitumia barabara hiyo.
Wakati vurugu hizo zikiendelea, wafugaji wa jamii ya Kimasai wakiwamo wanawake na watoto walionekana kukimbilia kwenye kituo kidogo cha Polisi Dumila kwa lengo la kujihami na kupata msaada wa polisi kutokana na hofu ya kushambuliwa na wananchi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi aliyekuwepo kwenye eneo la tukio, mkulima aliyefahamika kwa jina Mauya Hamadi alisema kuwa wananchi wamelazimika kufanya vurugu hizo baada ya wafugaji wa jamii ya Kimasai kuingiza mifugo kwenye mashamba ambayo tayari yameshapandwa mazao na kufanya uharibifu.
Alisema kuwa tayari suala hilo walishalifikisha kwa uongozi wa kijiji, kata, wilaya hadi mkoa, lakini hakuna jitihada zozote zinazofanywa na viongozi, hivyo kulazimika kumtaka Mkuu wa Mkoa Joel Bendera, kwenda kuzungumzia suala hilo, ambapo hata hivyo mkuu huyo wa mkoa hakuwahi kufika eneo hilo hadi walipoamua kufanya maandamano hayo.
Kwa msahada wa Gazeti la MWANANCHI.co.tz

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: FUJO KILA KONA Magari Nyumba Pikipiki zachomwa moto
FUJO KILA KONA Magari Nyumba Pikipiki zachomwa moto
http://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=80944&stc=1&thumb=1&d=1359199630
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2013/01/fujo-kila-kona-magari-nyumba-zachomwa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2013/01/fujo-kila-kona-magari-nyumba-zachomwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy